Jumamosi , 15th Dec , 2018

Mchezaji Mohamed Issa ameruhusiwa kuanza mazoezi wakati akikaribia mwisho wa adhabu yake ya kufungiwa baada ya kubainika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya bangi.

Kikosi cha Yanga

Mohamed Issa baada kubainika kutumia dawa hizo alifungiwa kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9,2017 na adhabu kumalizika Februari 8, 2019.

Mohamed Issa

Pamoja na kuruhusiwa kuanza mazoezi Mohamed Issa haruhusiwi kucheza mchezo wowote ule zaidi ya kufanya mazoezi.

Mohamed Issa alifungiwa na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Africa (RADO)