Meja Jenerali wa jeshi anavyoiongoza AS Vita

Jumanne , 12th Mar , 2019

Association Sportive Vita Club (AS Vita), ilianzishwa mwaka 1935 na Rais wa klabu hiyo kwa sasa ni Meja Jenerali mstaafu wa jeshi la DR Congo, Gabriel Amisi Kumba.

AS Vita na Rais wao Gabriel Kumba

Kumba alichaguliwa kuwa Rais wa klabu hiyo mwezi Machi 27, 2017 hivyo kuelekea Machi 16, 2019 kwenye mchezo dhidi ya Simba atakuwa anakaribia kutimiza miaka 12 akiwa madarakani huku akiwa amefanikiwa kuifanya AS Vita kuwa moja ya timu tishio Afrika.

Moja ya vitu ambavyo Kumba anatajwa kufanikiwa zaidi katika klabu hiyo ni kuifanya ijitegemee kiuchumi na kuweza kusajili wachezaji wakubwa pamoja na kuwalipa vizuri akiwemo mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi ambaye ni Jean-Marc Makusu akiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 350.

Mbali na soka, AS Vita imefanikiwa kuwa na timu bora katika michezo mbalimbali ikiwemo, Basketball, Nantei na Volleyball huku yote yakisimamiwa na Meja jenerali mstaafu Gabriel Kumba.

AS Vita wanakuja nchini kucheza mchezo wa mwisho Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi D dhidi ya Simba ambapo kila mmoja anahitaji ushindi ili aweze kusonga mbele huku pia wakisubiri matokeo ya JS Saoura na Al Ahly huko Misri.

Kundi D kwasasa linaongozwa na JS Saoura wenye pointi 8, Al Ahly pointi 7, AS Vita pointi 7 na Simba wakiwa wa mwisho na pointi 6. Katika kundi hili kila timu inaweza kusonga mbele.