Jumamosi , 11th Jun , 2016

Mshambuliaji Lionel Messi ambaye amekuwa akionekana kama hana bahati sana akiichezea timu yake ya taifa ya Argentina ikilinganishwa na jinsi anavyofanikiwa akiwa na FC Barcelona hii leo ameanza kufuta mdudu huyo wa mkosi ndani ya Ajentina.

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi akishangilia moja ya mabao yake 3 aliyofunga dhidi ya Panama.

Messi ameonyesha ubora kwake kwa kufunga mabao matatu yaaani hat - trick ndani ya dakika 19 akitokea benchi wakati timu yake ya taifa ya Argentina ikiipiga mkono Panama.

Mshambuliaji huyo alianza kufunga dakika saba tu tangu aingie akitokea benchi ambapo mshambuliaji huyo wa Barcelona alipokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wakati akiingia dimbani.

Messi alifunga bao jingine na akaongeza la tatu ndani ya dakika 10 za mwisho za mchezo huo.

Mabao mengine ya Argentina ambayo yalikamilisha idadi ya mabao matano katika mchezo huo yalifungwa na beki kisiki wa timu hiyo Nicolas Otamendi kwa kichwa safi huku linguine likikwamishwa hewani na Sergio Kun Aguero. 

Argentina sasa kwa ushindi huo inafikisha alama sita nakuongoza kundi D lenye timu za Chile, Panama na Bolivia.