Messi amkataa Ronaldo

Jumatatu , 12th Feb , 2018

Nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amesema yeye na nyota wa Real Madrid Criatiano Ronaldo hawawezi kuwa marafiki wala hafikirii kama itakuwa hivyo baada ya wote kustaafu.

Pamoja na Ronaldo kuwahi kunukuliwa akisema huenda watakuwa marafiki huko mbeleni, lakini Messi amesema hawana ukaribu hivyo ni ngumu wao kuwa marafiki.

"Sijui kama tutakuja kuwa marafiki, maana urafiki unajengwa kupitia kukaa pamoja na kujuana lakini sisi hatuna hiyo nafasi '', amesema.

Aidha messi amesema wachezaji hao hawana tofauti kila kitu kipo sawa ila maisha yao hayaingiliani sana kila mtu ana mambo yake na mara nyingi wanaonana kwenye sherehe za tuzo na kwenye michezo ya El Clasco tu.

Msimu huu Messi amefunga mabao 20 pamoja na kutoa pasi za mwisho 10 kwenye La Liga na Ronaldo amefunga mabao 11 na kusaidia mengine manne.