Jumatano , 28th Oct , 2020

Liverpool iliongeza alama mbili na kwenda juu kileleni mwa Kundi D baada ya ushindi dhidi ya FC Midtjylland usiku wa kuamkia leo lakini hofu imezidi kutanda baada ya kumpoteza Fabinho kwa jeraha la msuli.

Mlinzi wa Liverpool, Fabinho(aliyevaa jezi namba 3) akiwa chini baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Midtjylland .

Mbrazil huyo, ambaye amejiunga na Joe Gomez katika safu ya ulinzi wa katikati tangu kuumia kwa Virgil van Dijk kwa jeraha kubwa la goti mnamo Oktoba 17.

Majogoo hao wa jiji walianza bila ya washambuliaji wake wenye ushawishi Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino, na wakajikuta wanashindwa kufanya jaribio la lango la wapinzani wake katika kipindi cha kwanza.

Mafanikio ya Liverpool yalionekana baada ya Trent Alexander-Arnold kucheza namba mbili pamoja na ingizo la Xherdan Shaqiri, Diogo Jota kufanya makubwa katika mchezo hu Na wapinzani wa kundi Atalanta na Ajax wakitoka sare ya 2-2 huko Italia, Liverpool wana alama sita kutika michezo miwili.

Matokeo ya mechi za makundi mengine ni kwamba kundi B, Borussia Monchegladbach walitoka sare ya bao 2-2 na Real Madrid, Shaktar Donestk walitoka suluhu na Inter Milan.

Kundi A, Mabingwa watetezi Bayern Munich walipata ushindi wa pili baada ya kuilaza Lokomotive Moscow bao 2-1, nayo Atletico Madrid ilipata ushindi wake wa kwanza kwa kuilaza Fc Salsburg bao 3-2.

Katika kundi C, Fc Porto iliamka usingizini kwa kuilaza Olimpiacos bao 2-0, nayo Manchester City iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuitandika Marseille bao 3-0 ikiwa ugenini.

Michuano hiyo itaendelea leo ambapo kundi E itashuhudiwa Fc Krasnodar ikikipiga dhidi ya Chelsea, Sevilla itakua wenyeji wa Rennes.

Katika kundi F Borussia Dortmund itakabiliana na Zenit St Petersburg nayo Club Brugge watapepetana na Lazio. Kundi G patashika itakua baina ya Ferencvaros itaikabili Dynamo Kyiv na Juventus itapepetana na Barcelona.

Psg itakua ikijiuliza ugenini dhidi ya Instanbul Basaksehir nayo Manchester United itakua nyumbani kucheza dhidi ya RB Leipzig.