Jumapili , 2nd Oct , 2022

Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa
(SHIMIWI) 2022, yanaendelea kupamba moto Oktoba 2, 2022 jijini Tanga kwa michezo
mbalimbali kutimua vumbi ikiwemo mpira wa netiboli, mchezo wa kuvuta kamba kwa
wanaume na wanawake na mpira wa miguu.

Mchezo wa Kamba ndiyo ulikuwa fungua dimba kwa mashindano hayo kwa
sharamshamra huku timu zikivutana kwa kuonesha wamejiandaa ipasavyo na
kuonesha umahiri wao.

Timu ya Idara ya Mahakama wanaume ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanza mchezo huo
katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara kwa kuwavuta timu ya Tume ya Haki za
Binadamu kwa 2-0, Ofisi ya Rais Ikulu waliwavuta Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
kwa 2-0 na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) waliwavuta Tume ya
Maadili ya Viongozi wa Umma kwa 2-0.

Timu nyingine za mchezo huo wanaume ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
imepata ushindi wa 2-0 baada ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kutoingia
uwanjani, timu ya Bunge imewavuta Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa 2-0 na
timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera imewavuta timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga
kwa 1-0, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamepata alama 2-0
naada ya timu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutokufika uwanjani na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi iewavuta timu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa
2-0.

Kwa upande wa wanawake katika mchezo wa Kamba timu ya Idara ya Mahakama
imewavuta timu ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa 2-0, timu ya Wizara ya Maji
imewavuta Wizara ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa 1-0, Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata ushindi wa 2-0 baada ya timu ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutofika uwanjani hapo na timu ya Wizara ya Kilimo
imewavuta timu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum kwa 2-0.