Jumatatu , 6th Jun , 2016

Mipango ya mashambulizi ya kigaidi iliyopangwa kufanyika kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) nchini Ufaransa, imezuiwa, kulinganana Mkuu wa Usalama wa Urusi.

Mipango ya mashambulizi ya kigaidi iliyopangwa kufanyika kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) nchini Ufaransa, imezuiwa, kulingana na Mkuu wa usalama wa Urusi.

Mkuu huyo wa usalama wa nchi, alisema raia wa Ufaransa, alikamatwa nchini Urusi mwishoni mwa mwezi uliopita, baada ya kufanya mawasailiano na makundi ya maharamia ili auziwe bunduki na mabomu, kwenda kushambulia sehemu za ibada za Waislamu na Wayahudi nchini Ufaransa, pamoja na majengo ya Serikali na miundombinu, kama madaraja na reli.

Uwanja wa Taifa wa Ufaransa, Stade de France, ulikuwa moja ya maeneo yaliyolengwa kushambuliwa wakati wa mashambulizi ya Jijini Paris, yaliyoua watu 130, Novemba 13 mwaka uliopita.