
Straika wa Geita Gold, George Mpole
Mpole alifunga bao lake la ushindi dakika 11 ya mchezo wakati timu yake ikitoka sare ya 1-1 na Coastal Union katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Geita Gold ilikuwa ya kwanza kupata bao hilo kabla ya Rashid Chambo kuisawazishia Coastal Union dakika ya 19 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare na kumwachia Mpole kushinda kinyang'anyiro hicho baada ya Mayele kushindwa kufunga dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mpole kwa sasa anavuka rekodi ya mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyemaliza kinara wa ufungaji bora msimu uliopita wa 2020/2021 akifunga mabao 16.
Matokeo haya yanaifanya Coastal Union kumaliza msimu ikiwa nafasi ya saba na pointi 38 huku Geita Gold ikimaliza ya nne na pointi 46.