Jumamosi , 15th Dec , 2018

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika Mtibwa Sugar, wamesema wanelekea kwenye mchezo wao dhidi ya KCCA ya Uganda wakiwa hawana cha kulaumu kwani wamepokelewa vizuri sana.

Mtibwa Sugar

Mkuu wa msafara wa timu hiyo ambaye ni Mjumbe wa kamati ya shirikisho la soka nchini Steven Mguto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Coastal Union, amesema hakuna sababu ya kulalamika, wamepokelewa vizuri na wenyeji wao.

"Wenyeji wetu wametupokea vizuri sana, mpaka sasa hivi hatuna sababu ya kulalamika kwa sababu wametufanyia kila kitu ambacho tulikuwa tunahitaji kufanya hivyo tunaingia uwanjani kuiwakilisha nchi tukiwa vizuri kabisa'', amesema.

KCCA wanaongoza ligi kuu ya Uganda wakiwa alaama 24 kwenye mechi 11. Kwa ubora wa timu ya taifa ya Uganda ambayo imeshafuzu AFCON 2019 kutoka kundi L ambapo Tanzania pia ipo, inaelezwa kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.