Alhamisi , 2nd Sep , 2021

Bondia Namba Moja nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni siku ya kesho kutetea mkanda wake wa African Boxing Union dhidi ya Mnamibia Julius Indongo katika ukumbi wa Ubungo Plaza.

Hassan Mwakinyo akiunuliwa mkono na mwamuzi kutangazwa kuwa mshindi wa moja la pambano la ndondi la mwaka 2020.

Mwakinyo ni bondia namba moja kwa uzito wa uzani wa kati barani Afrika, akiwa na rekodi ya kutotoa sare, kashinda mapambano 19 huku 12 Akishinda kwa njia ya "Knock out" vilevile akiwaamepoteza mapambano mawili pekee. 

Pia Mwakinyo anashikilia mikanda ya WBF, UBO na WBL kwa uzani wa kati

Mwakinyo anaingia katika pambano Hili kutetea mkanda wake baada ya kumtwanga Antonio Mayala kutoka Africa Kusini, mwezi mei na kutwaa mkanda huo.

Kwa upande wa Indongo anarekodi ya kushinda mapambano 23 Kati ya 26 aliyocheza akipoteza mapambano matatu tu pekee. Pia Indongo ni Bingwa wa zamani wa dunia wa IBF, IBO, IBF kwenye uzito wa kati