
Mlinzi wa kati wa Simba, Ibrahim Ame akiwa mazoezini.
Mshika kibendera huyo, alionesha kiunua kibendera wakati kiungo wa Simba, Cleotus Chama anapiga kon ailiyozaa bao akiamini mpira huo ulitoka jambo ambalo limetafsiriwa na kamati hiyo kuwa sio sahihi kwa mujibu wa sheria za mpira.
Taarifa ya kamati hiyo iliyotolewa usiku wa kuamkia leo imeeleza kuwa, “Mwamuzi Gofrey Msakila ameondolewa katika ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kuumudu mchezo huo.
Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ta 40:1 (2.1) ya Ligi kuu kuhusu udhibiti wa waaamuzi”
Kwa upande mwingine:
Mchezaji wa Simba, Ibrahim Ame Mohammed nae amefungiwa michezo mitatu na faini ya shilingi 500,000 kwa kumzuia mwamuzi msaidizi asifanye kazi yake kwenye mchezo wa Gwambina dhidi ya Simba. Ame alimshika mkono mshika kibendera kumzuia asikiinue kuashiria kukashiria kupinga uamuzi wa mwamuzi huyo.
Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 39:5 (5.6) ya Ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.
Baada ya kushushiwa nyundo hiyo, Ame ataikosa michezo dhidi ya Yanga, Coastal Unioni na KMC ya VPL.