Ijumaa , 12th Dec , 2014

Shirikisho la Soka nchini TFF limesema wanawake nchini wameendelea kupiga hatua katika soka hususani kwa upande wa waamuzi.

Akizungumza na East Africa Radio, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Eliud Mvela amesema katika mechi ya Nani Mtani Jembe inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Wiki hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo itashirikisha Timu za Simba na Yanga, mwanamke ndiye atakuwa mwamuzi wa kati na wanaamini anauwezo wa kuchezesha mechi hiyo.

Mvela amesema wanawake nchini wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kushiriki kozi mbalimbali za uwamuzi ili kuendelea kukuza soka zaidi hapa nchini.