(Mchezaji wa Namungo Shiza Kichuya akijaribu kumpita mlinzi wa Geita Gold.)

(Idadi ya magoli iliyofungwa kila timu katika mzunguko wa kwanza ligi kuu Tz bara)
Ikumbukwe mzunguko wa kwanza ulikamilika huku klabu yanga ikiwa ndio timu iliyofunga magoli mengi zaidi ikiwa imefunga jumla ya magoli 25 na pia ndio timu iliyofungwa magoli machache magoli zaidi, ikiwa imefungwa magoli manne pekee.
Na mahasimu wao klabu ya Simba ikiongoza kwa timu zilizoshinda michezo mingi ya uwanja wa nyumbani, ikiwa imeshinda michezo 6 kati ya michezo 8, na Yanga ikiwa timu iliyoshinda michezo mingi ugenini ikishinda michezo 7 kati ya michezo 9. Na klabu ya Ruvu shooting ikiwa ndio timu ilyofungwa magoli mengi zaidi ikifungwa jumla ya magoli 21 katika michezo 15.
Ligi hiyo itaendela kesho kwa michezo miwili ambapo mbeya kwanza watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika Dimba la Sokine jijini Mbeya majira ya saa kumi jioni, huku watoto wa kinondoni klabu ya KMC ikiminyana na maafande wa polisi Tanzania majira ya saa 1 usiku katika dimba la Azam Comlpex Chamazi jijini Dar es salaam.
Na Michezo ya jumapili ni Ruvu shooting dhidi ya Dodoma jiji saa 8 mchana, Tanzanaia Prisons dhidi ya Mbeya City saa 10 jioni, na Yanga dhidi ya Kagera sugar saa 1 usiku.


