Jumanne , 1st Feb , 2022

Uongozi wa klabu ya Yanga umekiri kuhitaji alama tatu katika mchezo wao ujao  wa ligi kuu  dhidi ya  Mbeya City utaopigwa Februari 5, 2022 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

(Fiston Mayele akishangilia goli na Feisal Salum)

Hayo yamesemwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddien Nabi amabye amesema wanachohitaji kwenye mchezo huo ni pointi tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kumaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi nzuri. 

“Kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu na ili kupata pointi ni lazima tushinde mchezo wetu licha ya kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inafanya kazi kubwa kusaka pointi tatu hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja kutupa hamasa ,” Alisema Nasreddien.

Kikosi cha Yanga  yenye pointi  ikiwa nafasi ya kwanza na alama 35 huku Mbeya City ipo nafasi  ya nne katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC.