Nadal na Federer wapidhana US Open

Jumatano , 5th Aug , 2020

Bingwa wa michuano ya Us Open Rafael Nadal amejitoa katika michuano hiyo kwa kile alichodai kuwa ni tahadhari dhidi ya Covid-19.

Nyota wa mchezo wa Tenisi Duniani Rafael Nadal akiwa na moja ya taji la michuano hiyo.

 

Nadal alikua amebakiza taji moja tu ili kufikia rekodi ya Rodger Federer ya Grand Slam nyingi na wengi waliamini huenda hii ndio nafasi ya kumkuta Federer lakini itakua tofauti.

Kwa maamuzi hayo itambidi Nadal kusubiri hadi michuano ya French Open ili kuweza kumfikia Federer.

Mara ya mwisho kutoshuhudia Federer na Nadal katika Grand Slam ilikua mwaka 1999 na sasa ni mara ya kwanza,na sasa ni baada ya miaka 21 tunaenda tena kuona Grand Slam bila mmoja kati ya wakali hao.