Alhamisi , 2nd Oct , 2025

Mchezaji nyota wa timu ya Minnesota Lynix inayoshiriki ligi ya mpira wa kikapu upande wa wanawake nchini Marekani (WNBA) Napheesa Collier amefunguka kuwa uongozi wa ligi hiyo ambao unaongozwa na Cathy Engelbert umekua na utaratibu mbovu ,waamuzi kutochezesha kwa haki.

Napheesa Collier

Pia wachezaji nyota wa timu tofauti kupitia mitandao yao ya kijamii wamemuunga mkono nyota huyo akiwemo Angel Reese, Lexie Hull, Isabelle Harrison na kocha mkuu wa timu ya Indiana Fever Stephanie White ambapo anasema maoni ya Napheesa Collier yamekuja wakati sahihi.

Ikumbukwe septemba 10 kamishna huyo  wa WNBA alisema timu ambazo zinatoa maoni mabaya kuhusu waamuzi wa mchezo ni wale walioshindwa kufanya vizuri msimu huu, na kuhusu mshahara kwa Caitlin Clark, Angel Reese WNBA inawapa nafasi ya kuonekana wanatengeneza pesa nyingi nje ya uwanja.