Jumamosi , 23rd Jan , 2016

Kiungo kinda wa klabu ya Simba Said Ndemla, anatarajia kwenda kufanya majaribio kwenye kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo ili kusaka nafasi ya kucheza soka katika klabu hiyo.

Kiungo wa Klabu ya Simba SC Said Ndemla

Jamali Kisongo ambaye ni meneja wa Mbwana Samatta, amesema kuwa, ataendelea kuwasaidia wachezaji wa Tanzania kupenya kwenye soka la kimataifa kama Samatta.

Kisongo amesema, amewapeleka Ubwa na Chanongo kufanya majaribio TP Mazembe na kinachoendelea sasa ni mazungumzo kati ya Stand na Mazembe kwa ajili ya usajili.

Kisongo amesema, anampeleka Ndemla akafanye majaribio lengo likiwa ni kuwasaidia wachezaji wengi wa hapa nyumbani kupata fursa ya kucheza soka nje ya mipaka ya nchi.

Kisongo amesema, mbali na Ndemla pia kiungo wa Mtibwa Sugar Mohammed Ibrahim naye anahitajika baada ya awali safari yake kushindikana.

Hivi karibuni, watanzania, Abuu Ubwa na Haruna Chanongo walienda kufanya majaribio Mazembe ambapo kwa sasa hatua iliyobaki ni makubaliano kati yao na Stand United inayowamiliki wachezaji hao.