Jumatatu , 17th Aug , 2020

Baada ya timu ya Newcastle United kushindwa kuuzwa kwa mfanyabiashara wa familia ya kifalme ya Saudi Arabia, kutokana na kile kilichoelezwa historia ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu toka katika familia hiyo katika utawala wake,hivi sasa Timu itauzwa kwa matajiri kutoka nchini Singapore.

Mmiliki wa timu ya Newcastle Mike Ashley (Pichani) akitafakari jambo.

Mike Ashley ambaye ndiyo  Mmilikiwa timu hiyo mwishoni mwa mwaka  2017 alitangaza kuiweka sokoni timu yake ilikupata  mmiliki mwingine bila mafanikio hadi mwaka  2020 alipojitokeza Mfanyabiashara Prince Mohamed  bin Salmin kutoka Saudi Arabia aliyekusudia kuichukua klabu hiyo.

Baada ya kushindikana.Mwana wa mfalme Bin Salmin alikata tamaa hadi ilipojitokeza kampuni nyingine Bellagraph Nova Group (BNG) ya Singapore ambayo haijaripotiwa kuwa na  kashfa ambazo zilikua kikwazo wa ununuzi wa awali kufanyika.

Kama mpango huu utafanikiwa basi huwenda ukaongeza ushindani mkubwa kwenye  ligi ya  ya England kama ilivyokuwa kwa  Chelsea na Manchester City kufanya  mapinduzi makubwa ya kiushindani baada ya kununuliwa na  Matajiri wa Mataifa mengine.