
Wachezaji wakongwe mbalimbali (kwenye duala jeusi ni Claude Makélélé.
Makelele ameeleza kuwa Pogba hastahili kufanya hivyo mbele ya wapinzani wake kwani sio jambo la busara kimichezo.
"Kumfunga mpinzani wako goli 4 kisha unacheza mbele yake baada ya mchezo sio jambo la hekima kwa mpinzani hata kidogo. Huko ni kudharau wapinzani wake aliowafunga", ameeleza Makelele.
#EPL FT
Mchezo umemalizika kwa Man United kupata ushindi wa tatu mfululizo chini ya kocha Ole Gunnar SolskajeManchester United 4-1 Bournemouth
Pogba 5' 34' Ake 45+2'
Rashford 45'
Lukaku 72' pic.twitter.com/YZvak4b1E9— East Africa TV (@eastafricatv) December 30, 2018
Makelele amesisitiza kuwa kila mchezaji huwa anafurahi anapopata ushindi au kufunga bao lakini mambo kama hayo ayafanye kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Tangu kuondoka kwa Jose Mourinho na kuteuliwa kwa Ole Gunnar Solskjær Pogba amekuwa kwenye wakati mzuri akifunga mabao 4 na kusaidia matatu kwenye mechi 3 walizocheza mpaka sasa.