Anthony Elanga akishangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la kusawazisha
Elanga mwenye umri wa miaka 19 aliingia kwenye mchezo huo dakika ya 75 akichukua nafasi ya Marcus Rashford, na dakika 5 baadae akaifungia Manchester United bao la kusawazisha dakika ya 80 katika mpira wake wa kwanza kugusa kwenye mchezo huo.
Baada ya mchezo huo kijana huyo raia wa Sweden akaeleza namna alivyopewa maelekezo na kocha mkuu Ralf Rangnick namna ya kucheza mpaka kutimiza ndoto yake ya kufunga kwenye michuano hii,
"Koch aliniambia niwafanye mabeki waogope na nikimbie nyuma yao napo pata nafasi. Nimekuwa na ndoto na nyakati kama hizi, kufunga katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu za juu za Ulaya kama Atletico Madrid, ndoto imetimia." Amesema Elanga
Hili ni bao la 4 kwa kinda huyo msimu huu akiwa na Manchester united katika michezo 16 kwenye mashindano yote. Kwenye mchezo huo Atletico Madrid ndio walikwa wa kwanza kupata bao dakika ya 7 kupitia kwa Joao Felix. Timu hizi zitacheza mchezo wa mkondo wa pili Machi 15, 2022.


