Ijumaa , 25th Jan , 2019

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema yeye ataendelea kuhakikisha kiasi kidogo kinachopatikana kutoka kwa mashabiki kinakwenda kwa wachezaji kwani yeye anajua pesa zake atalipwa tu.

Mwinyi Zahera

Zahera ameiambia Kipenga Xtra ya East Africa Radio kuwa yeye hawezi kukubali apate pesa wakati wachezaji hawana hela hivyo lazima wao wapate kwanza ndio yeye afuatie.

''Kuna muda viongozi wanataka mimi nisafiri kwa ndege kwenda mikoani kwenye mechi lakini mimi nasema hapana lazima wachezaji ndio wasafiri kwa ndege maana sichezi mimi wao ndio wanakwenda kucheza'', alisema.

Kuhusu yeye kulipwa pesa zake, Zahera amesema hana wasiwasi kwani anamkataba hivyo atalipwa tu hata baada ya miaka 10 na kama ikitokea hawatamlipa atawapeleka FIFA na atapata haki yake.

Zahera ameiongoza Yanga kupata matokeo mazuri msimu huu ambapo katika mechi 20 za ligi imefungwa mchezo mmoja tu na kujikusanyia alama 53 katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.