Alhamisi , 22nd Apr , 2021

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ilimlazimu kuzungumza na mashabiki walioingia kwenye uwanja wao wa mazoezi huko Carrington mapema leo waliokuja na ujumbe wa kupinga umiliki wa familia ya Glazer kwenye klabu hiyo.

Baadhi ya mashabiki wa Manchester United waliojitokeza kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Carrington

Makumi ya mashabiki waliingia kwenye uwanja huo wakiwa na mabango yaliyosema 'Glazers Out' na mengine yaliandikwa '51% MUFC'

Mwenyekiti mtendaji wa Man.utd Joel Glazer ndio alikuwa makamu mwenyekiti wa European Super League kabla ya United kujiondoa ushiriki Jumanne wiki hii baada ya michuano hiyo kupingwa vikali na wadau pamoja na mashabiki wa soka duniani kote kwa akuonesha vitendo vya hasira kali za kuchukizwa na mashindano hayo.

Siku ya Jumatano Glazer alitoa barua ya kuomba msamaha na kukiri kwamba uongozi wa Timu ulifanya makosa kujiunga na mashindano hayo yaliyo pendekezwa kwa lengo la kuviongea kipato vilabu. United walikuwa moja ya vilabu sita vya Ligi Kuu ya England kujiandikisha kishiriki European Siper league, kabla ya wote kujitoa ndani ya masaa 48 baada ya mashindano hayo kutangazwa.