bondia Dillian Whyte
Whyte mwenye umri wa miaka 33,ambaye anakamata nafasi ya kwanza kwa rekodi ya WBC ndiye mpinzani halisi wa Tyson Fury anayemiliki mkanda wa WBC. Fury mwenye miaka 33 ametupia kijembe kwenye mtandao wake wa kijamii baada ya mpinzani wake Dillian Whyte kusaini mkataba wa pambano lao kuwa amesaini mkataba ambao hajawahi kulipwa na hatoweza kuja kulipwa kwa fedha alizopewa kisa kukubali kucheza na yeye.
Pambano hilo linaloandaliwa na promota Frank Warren ambaye alishinda tenda ya kuandaa pambano hilo kwa kuweka kiasi cha dollar million 41 (sawa na billion 94,874,000,000 za kitanzania) huku bondia Tyson Fury akitarajiwa kupokea asilimia 80% huku mwenzake Dillian Whyte akitarajiwa kupokea asilimia 20% kilichobakia kwenye pambano hilo.

