Jumatatu , 1st Mar , 2021

Rais wa zamani wa Barcelona Jose Maria Bartomeu anashikiliwa na polisi nchini Hispania baada ya kuhusishwa na tuhuma ya kurubuni makampuni mbalimbali ya mitandao ya kijamii kuandaa kampeni maalum ya kuwashambulia watu na taasisi zilizokuwa zinapinga utawala wa Rais huyo.

Rais wa zamani wa Barcelona, Jose Maria Bartomeu.

Rais huyo ambaye alihudumu kwenye klabu hiyo kwa miaka 6 tokea mwaka 2014 hadi kujiuzuru kwake Oktoba mwaka jana, amekamatwa baada ya maafisa hao wa usalama kutembelea ofisi za klabu hiyo kwa ajili ya kusaka nyaraka muhimu zitakazo husika kwenye tuhuma hizo.

Baadhi ya makampuni yalitajwa kuhusika kwenye  tuhuma hizo ni NSG Social Science Ventures SL, Tantra Soft SA, Digital Side SA, Big Data Solutions SA and Futuric SA nah ii ni kwa mujibu wa jarida la michezo la kuaminika nchini Hispania la ‘Marca’.

Licha ya kushikiliwa na polisi, lakini Bartomeu alikana kuhusika kwenye tuhuma hizo mwezi Juni maka jana.

Hii ni mara ya pili polisi hao kutembelea ofisi za klabu ya Barcelona na kufanya ukaguzi kuhusiana na kesi hiyo, kwani mwishoni mwa mwaka jana Jaji wa Mahakama inayosimamia kesi hiyo aliamuru klabu ikaguliwe na leo wamekagua kwa mara ya pili.