(Marcus Rashford)
Rashford anaonekana kutokua na furaha ndani ya Manchester united kwasasa, baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Ralf Rangnick na sasa anatafakari hatima yake kama ataendelea kusalia old trafford ama ataamua kuihama klabu hiyo msimu ujao.
Mustakabali wa Rashford unazidi kutokuwa na uhakika na kuleta wasiwasi kwa wapenzi wa klabu hiyo kwasababu mchezaji huyo anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake ambao utamalizika majira ya joto mwaka 2023, huku kocha Mauricio Pochettino akithibitisha kumuhitaji Rashford lakini amesema kama yeye atafanikiwa kupata nafasi ya kuwa kocha wa Manchester United msimu ujao basi angependa Rashford abakie huko huko ili msimu ujao afanye nae kazi katika viunga vya Old Trafford.
Na vyanzo vya habari vya nchini England vinasema Rashford anafanya mazoezi vizuri na yuko katika ari nzuri ya ushindani na bado hajafanya maamuzi yoyote na amelenga kurejesha kiwango chake cha juu ili kurudisha nafasi yake katika kikosi cha kwanza japo pia hana uhakika wa kusaini mkataba mpya na United, ambao wanatamani sana kumbakisha na hawataki kumpoteza kwa uhamisho wa bure.
(Cristiano Ronaldo na Edinson Cavani)
Vile vile baada ya Cristiano Ronaldo kutojumuishwa katika kikosi kilichocheza dhidi ya Manchester City mwisho wa wiki iliyopita, kuna taarifa kwamba Ronaldo anaungana na Edinson cavani pamoja Anthony Martial kua katikaorodha ya wachezaji wanoa fikiria kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.





.jpg?itok=5cvL0YaP)