Wawakilishi wa timu shiriki wakishuhudia droo pamoja na kupata semina maalum kuelekea michuano hiyo
Michuano hiyo itakayoshirikisha timu 52 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 2 jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya mechi 13 za awali zitapigwa kwa mtindo wa mtoano ikiwa ni safari ya kutafuta timu 16 bora.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Meneja Meneja Masoko na Mauzo kutoka East Africa Television LTD, Roy Mbowe amesema lengo la kuendesha droo hiyo ni kutaka kuweka uwazi na ukweli katika michuano hiyo.
"Mambo yetu yatakuwa yanakwenda 'live' ili muweze kuona mwenyewe kinachoendelea msije kusema wamependelewa timu flani kupangwa na flani ndiyo maana tukawaita hapa muone na kuchagua wenyewe droo hii na baada ya hatua ya mchujo timu zitapangwa kwa droo iliyo wazi kwa kuzingatia aina ya ushindi zilizopata ili kupata timu 16 bora zitakazoendelea mashindano". Alisema Roy
Aidha, Roy amewataka wachezaji wawe na nidhamu katika michuano hiyo ili waweze kuonesha kile walichonacho zaidi katika michuano hiyo.
"Timu au mtu yeyote atakaye anzisha fujo na kusababisha mchezo kuvunjika, itaondolewa au ataondolewa mashindanoni..Timu itapoteza michezo yake, michezo inayosalia timu husika zitapata ushindi kwa mujibu wa sheria za FIBA na kanuni za TBF". Alisisitiza Roy
Meneja wa Masoko na Mauzo kutoka East Africa Television LTD , Roy Mbowe (Kulia), Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano TBF, Manase Zablon (Katikati), Gosbert Boniface - Technical Director Basketball
Naye Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji wa Mashindano wa TBF Manase Zablon amewasihi wachezaji wote kwa ujumla kuzingatia kanuni za mchezo zilizowekwa katika mashindano hayo ili kuweza kuupa hadhi mchezo huo kwani tangu kupatikana kwa uhuru nchini Tanzania hakuna shindano la mpira wa kikapu lolote lililoweza kuweka zawadi nono kama waliyoitoa Sprite ambayo ni shilingi milioni 15.
MATOKEO YA DROO
Hii ndiyo ratiba kamili ya michuano ya Sprite BBALL KINGS itakayoanza kutikisa siku ya Jumamosi ya Juni 2 katika uwanja ambao utatangazwa baadaye....
Home Away
1. God with us Vs Oiler
2. The Action Vs DMI
3. Team Brotherhood Vs Osterbay
4.Bahari Beach Vs Rock City Warriors
5. Celestial Vs Ukonga Warriors
6.Kampala Universty Vs Heroes B
7. Street Warriors Vs BIAS
8. External Warriors Vs Bios Stars
9. Bongo Hits Vs Lord Baden
10. Mchenga Team Vs Wazawa Team
11. Makongo Juu Vs Kigamboni Heroes
12. Flying Dribblers Vs Ustawi wa Jamii
13. Yo! Street Vs K- Warriors
14. K.K Squad Vs TMT
15. Mj Junior Vs Land Force
16. Junior Club Vs Kurasini Heat
17. Lycans Mbezi Beach Vs The Fighter
18. Ardhi Universty Vs Street Boys
19. Dandy Vs UDSM
20. St Joseph Vs Raptors
21. Panorama Vs No Name
22. Dream Cheaser Vs King Juniors
23. The Heroes Vs T-Kimanga
24. Cavallie Vs Chanika Legend
25. Weusi Vs Port Land
26. Force one Vs St. Mont Fort