Jumatatu , 8th Mar , 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema anaandaa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Songwe ili kugawana takwimu za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi VVU kama walivyogawana mali na vitu vingine wakati wanaugawa Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akiongea

Takwimu za mambukizi ya VVU Mbeya kwa sasa ni asilimia 9.

Chalamila ameyasema hayo leo Machi 8, 2021 wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Ameeleza kuwa wakati wanaugawa Mkoa wa Mbeya waligawana mali na vitu vingine lakini takwimu za Ukimwi hawakugawana hivyo kuufanya Mkoa wa Mbeya kuwa na takwimu za juu kuliko zingegawiwa.

"Tutafanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Songwe ili kuwagawana hizi takwimu za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi maana wakati Mkoa wa Mbeya ukigawanywa takwimu zilibaki kwetu, hivyo lazima tugawane kama vitu vingine tulivyovigawa na utasaidia Mbeya kuwa na idadi ndogo ya maambukizi kuliko ilivyo sasa'', amesema Chalamila.