Kuelekea kwenye mchezo huo Makocha wa Wasaidizi wa klabu za Yanga na KMC wamekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini kila mmoja akijinasibu kuondoka na alama tatu muhimu baada ya dakika 90.
'Ukiachana na michezo hiyo wanaotufuata nyuma wanapambana ili nao waweze kuja juu, lakini tumejipanga kufanya vizuri na hali ya kikosi ipo vizuri, wachezaji wetu ambao walikuwa majeruhi wamerejea kwa ajili ya kupambana ili kumaliza katika nafasi nzuri ''
Yanga SC ndiye kinara wa Ligi Kuu NBC Tanzania akiwa na alama 59 ilhali KMC FC ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama zak3 23. Kwenye michezo 9 waliyokutana KMC imeshinda mara 1 tu tena mwaka 2020 huku ikifungwa na Yanga SC mara 6 na kutoa sare 2.






