Ronaldo mfalme wa mabao Ulaya

Thursday , 14th Sep , 2017

Usiku wa Ulaya umeendelea usiku wa kuamkia leo kwa kukamilisha mechi 16 za ufunguzi wa hatua ya makundi.

Mabingwa watetezi Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Apoel. Mabao mawili kati ya hayo yakifungwa na Cristiano Ronaldo na kumfanya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi katika UEFA pekee akiwa na mabao 107.

Liverpool wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare ya 2-2 na wababe wao wa fainali ya EUROPA 2016 Sevilla. Huku Manchester City chini ya kocha mshindi wa UEFA mara mbili Pep Guardiola wakiiadhibu Fayenood ya Uholanzi mabao 4-0.

John Stone mlinzi wa kati wa Manchester City amejiwekea rekodi ya kuwa mlinzi wa kwanza kufunga mabao mawili sawa na Lionel Messi na Ronaldo katika hatua ya makundi Tottenham wakiwa Wembley wamelipiza kisasi kwa Borrusia Dortmund baada ya kuwachapa 3-1 Wajerumani hao.

Gabriel Jesus wa Man City ameungana na Romelo Lukaku kwenye orodha ya wachezaji waliofunga katika mchezo wao wa kwanza wa UEFA.