Jumamosi , 13th Nov , 2021

Taarifa za ndani kutoka Barcelona vimeripoti kuwa, sababu za kumrejesha Dani Alves Barcelona ni kutaka nyota huyo aongeze uzoefu kwa wachezaji wenye umri mdogo waliopo kikosini hapo pamoja na kuwajengea uwezo.

(Dani Alves akishangilia na kocha wake wa sasa Xavi Hernandes walikuwa wanacheza wote kuanzia 2008-2016)

Alves mwenye miaka 38 kwasasa, amerejea Barcelona baada ya taarifa zilizothibitishwa na klabu hiyo Novemba 12, 2021 usiku zilizoeleza kuwa, Alves atakuwepo klabu hapo hadi mwisho wa msimu huu wa mwaka 2021-2022 na atapokea Euro 1 sawa na shilligi 2600 za kitanzania ili asiwaumize Barcelona yenye hali mbaya ya kiuchumi.

Licha ya kusajiliwa akiwa mchezaji huru, Alves hatoruhusiwa kuichezea klabu hiyo ya zamani hadi dirisha dogo la mwezi Januari lifunguliwe kutokana na sheria za kawaida za usajili wa La Liga na shirikisho la Soka Duniani FIFA.

Alves ataungana na nahodha wake Xavi Hernandez ambaye kwasasa ndiye kocha wa Barcelona ili kuwaongezea uwezo wachezaji wenye umri mdogo kikosini, kuwaambukiza ari ya ushindi na kuwaonesha kuwa yeye ni kiongozi wa mfano.

Kwasasa Barcelona ina mlinzi wa kulia mmoja asilia, Mmarekani Sergino Dest licha ya kuwatumia Oscar Mingueza na Sergio Roberto kama walinzi wa kulia pale inapobidi jambo linalotazamiwa kumpa fursa Alves ya kucheza zaidi.

Alves ambaye kwasasa ndiye mchezaji mwenye mataji mengi zaidi kwenye historia ya soka, mataji 46 huku mataji 26 akiyabeba akiwa Barcelona kuanzia msimu wa mwaka 2008 hadi aliondoka mwaka 2016 na kutimkia Juventus.

Mkongwe huyo mwenye uhodari wa kushambulia zaidi akiwa  mlizni wa kulia, alifanikiwa kucheza michezo 391, kufunga mabao 21 na kutoa Assist 101 kwenye michezo yote alipokuwa Barcelona.

Nyota huyo alishafungua milango ya kurudi Barcelona tokea mwezi Septemba 2021 alipoachana na Sao Paolo na kusema atarejea kama klabu ikimtafuta na kuhisi anacho chakkiongeza klabuni.