Mbele ya wanahabari Mbwana amesema kuwa matokeo ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Lesotho siyo mashabiki pekee walioumizwa bali hata wao wachezaji kwa kuwa matokeo hayo yanawaweka sehemu mbaya katika hatua hii ya makundi.
“Mimi sipendagi kushindwa, hata droo sijaifurahia kwa sababu tulikuwa tunacheza nyumbani na ukizingatia ni hatua ya makundi tulikuwa tunahitaji ushindi kwa lazima kwa hiyo tumepata droo sio mbaya lakini haikuwa katika akili yangu kwamba tupate droo dhidi ya Lesotho nyumbani wakati tulikuwa tunahitaji ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kundi.” Samatta alifunguka.
Aidha Samatta ameongeza kwamba “Nafikiri wachezaji wote walikuwa na hasira sio mimi peke yangu labda nilishindwa kujizuia kutoionesha lakini hakuna mtu ambaye amefurahia matokeo haya.”