
Kocha Mbrazil Luis Felipe Scolari
Scolari alisema '' Anelka alikuwa mchezaji mzuri na alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga tatizo lake alikuwa anacheza nafasi moja tu kiwanjani, hakuwa na mahusiano mazuri na Drogba hivyo ilikuwa ngumu kuwatumia wote kwa pamoja''
'Suala lililopandikiza chuki iliyoleta utovu mkubwa wa nidhamu na kutokuheshimiana miongoni mwetu na kazi kuharibika kwa upande wangu kutokana na wachezaji hawa kuwa vipenzi vya mmiliki wa timu Roman Abrahimovich'' alimaliza kusema.
Kocha Scolari alijiunga Chelsea iliyoshehena nyota kadhaa mwaka 2008 kuchukua nafasi ya Avram Gram na kudumu kwa miezi 7 tu,kabla tajiri wa timu Abromavich kumtimua na kumleta Carlo Anicellot ambaye alifanikiwa baada ya kulazimisha washambuliaji hawa kucheza kwa pamoja.
Luis Scolari kocha mshindi wa kombe la dunia mwaka 2002 kule Japan na Korea, amekuwa na mafanikio kadha makubwa kwenye soka pamoja na ukweli amekuwa na msuguano na nyota timu anapokuwa kwenye timu.
Wengi wanamkubuka zaidi kwa mafanikio ya kutwaa kombe la dunia 2002 ambapo pia wakati wa uteuzi alimuacha nyota wao Romario na kumteua kwa mara ya kwanza Ronaldinho Gaucho hali iliyozua mjadala mkubwa sana.
Mwaka 2014 alirudi tena katika timu ya taifa ya Brazil ambapo pia walikuwa wenyeji wa fainali hizi akaishia kwenye aibu ya kufungwa 7-1 na Wajerumani katika hatua ya nusu fainal