Jumamosi , 25th Mei , 2019

Sherehe za kukabidhiwa kombe kwa klabu ya Simba zimeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha leo jijini Dar es salaam hivyo kuharibu utaratibu wa namna ya kutembeza kombe.

Mechi ya Simba na Biashara ikiendelea uwanja wa taifa.

Imeelezwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa Dar es Salaam itawakosesha wanasimba uhondo wa kukabidhiwa kombe lao la ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2018/19.

Kwa mujibu wa pende zote mbili yaani Simba na shirikisho la soka Tanzania (TFF), sasa sherehe hizo zitafanyika mkoani Morogoro siku ya Jumanne tarehe 28, 2019 watakapocheza na Mtibwa Sugar.

Mchezo wa Simba dhidi ya Biashara United leo umemalizika kwa sare ya 1-1, huku ukitawaliwa na mvua kubwa na kama sio miundombinu bora ya uwanja wa taifa pengine mchezo ungeahirishwa.