Simba bingwa wa Ligi kuu Tanzania bara 2019/20

Jumapili , 28th Jun , 2020

Klabu ya Simba SC imetwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya mchezo uliomalizika jioni ya leo juni 28, 2020 kwenye uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya wakitoka suluhu na tanzania prison. simba imefikisha pointi 79 kwenye mechi 32 na haziwezi kufikiwa,

Kikosi cha Simba

na haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Simba SC wamefikisha pointi 79 kileleni kwenye mechi 32 hivyo haziwezi kufikiwa na timu yoyote haswa baada ya Jana Juni 27, 2020 Azam FC kutoka sare na Biashara United, ambapo walitakiwa kushinda mechi zao 7 ili wakusanye alama 21 na kufikisha pointi 79 huku wakiomba Simba wapoteze mechi zote.

Simba sasa wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa misimu mitatu mfululizo na huu ni ubingwa wa 21 kwa kwao katika historia ya ligi kuu soka ya Tanzania bara.

Pamoja na ubingwa huo, mshambuliaji Meddie Kagere ndiye anayeongoza orodha ya wafungaji mpaka sasa akiwa na magoli 19.

Kagere naye anatafuta tuzo ya ufungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kuibuka mfungaji bora akiwa katika msimu wake wa kwanza tu aliposajiliwa na Simba kutoka Gor Mahia ya Kenya.