
Mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula.
Manula amerejea kikosini baada ya kupona maumivu ya kichwa aliyoyapata kwenye mchezo wa VPL uliopita dhidi ya JKT TZ kufuatia kugongana na mshambuliaji wa timu hiyo Daniel Ruben Lyanga hata kupelekea Manula kupoteza fahamu na kushindwa kuendelea na mchezo huo.
Licha ya kusafiri na kikosi cha Simba kwenda nchini Sudan timu yake hiyo ilipocheza dhidi ya Al-Merreikh na kupata sare ya bao 1, lakini mlinda mlango huyo bora nchini kwasasa hakuweza kucheza na badala yake nafasi yake kuchukuliwa na Beno Kakolanya.
Baada ya kuukosa mchezo huo, Kocha Didier Gomez da Rosa ameamua kumpanga mlinda mlango wake huyo chaguo la kwanza ili kumuwek afiti kabla ya kurejeana na Al-Merreikh tarehe 16 mwezi huu jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha mabingwa hao watetezi wa VPL kitakachotafuta nafasi ya kulipiza kisasi mbele ya TZ Prisons ni: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein(C), Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Perfect Chikwende, Mzamiru Yassin, Chris Mugalu, Rally Bwalya na Luis Miquissone.
Watakaoanzia benchi ni pamoja na Mlinda mlango, Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Thadeo Lwanga, Benard Morrison, Medie Kagere, John Bocco na Clatous Chama ilhali Hassan Dilunga, Ibrahim Ajib na Gadiel Michael hawapo kikosini kabisa.