Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati wakupitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022 nakuitaja moja ya sababu iliyosababishwa na TFF na kupelekea timu ya Simba kushindwa kimataifa kufuatia bodi ya Ligi kuiwekea mechi ya watani wa jadi ikiwa ni siku chache kabla ya kuivaa Kaizer Chiefs ambayo mnyama alinyukwa bao 4-0.
''Kwa mimi ninavyoangalia kwa jinsi nilivyoiangalia Simba, ilikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu.''
''Kuna mahali tumekosea, na tunakosea pale ambapo hatuweki vipaumbele, yani sisi mambo yote yapo sawa tu,kwamba mtu anaenda kucheza mchezo ambao unaweza kuleta kombe Tanzania kwa mara ya kwanza, kati kati yake unaenda kuwawekea mchezo mkubwa wa watani wa jadi.''
''Simba imeenda kucheza mchezo mkubwa Afrika Kusini bila Game Plan, wenyewe walikuwa wanawaza mechi ya watani wa jadi, hatukuwa na mpango.''
''Wapo watu wanalaumu eti Simba kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa eti ilihujumiwa na Senzo Mazingiza, kweli Yanga ambayo imewapa Benard Morrison tena hata nauli waliyomtumia kumleta hapa nchini hamjamlipia kweli iwahujumu dhidi ya Kaizer Chiefs.Kweli Simba iliyoifunga Al Ahly ije ihujumiwe na Senzo na mashabiki wa Yanga''?
''Timu zinazokwenda kwenye michuano ya kimataifa, zinaliletea sifa Taifa lazima bodi hizi zinazosimamia lazima wawape vipaumbele.''
-Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Mwigulu Nchemba .
