Simba kubadili nembo yake

Jumatatu , 17th Feb , 2020

Klabu ya soka ya Simba imeeleza nia yake ya kutaka kubadili nembo ya klabu hiyo.

Nembo ya klabu ya Simba

Simba ambayo imekuwa ikitumia nembo yenye rangi mbili kuu, nyekundu na nyeupe kwa muda mrefu, imesema kuwa kabla ya kuanza mchakato huo inahitaji kupata maoni mbalimbali ya mashabiki na wadau wa klabu hiyo.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Simba imeweka taarifa hiyo huku ikihitaji mashabiki wake kutuma maoni yao juu ya mabadiliko ya nembo hiyo katika email maalum.

Klabu ya Simba ilianzishwa mnamo mwaka 1936 na imekuwa ikibadili nembo hiyo mara kadhaa mpaka hivi sasa.