Alhamisi , 5th Dec , 2019

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa imefikia makubaliano na aliyekuwa kocha wa Polisi Tanzania Seleman Matola na sasa anakwenda kuanza kazi katika klabu hiyo kama kocha msaidizi.

Basi la klabu ya Simba

Akizungumza na Kipenga ya East Africa Radio, msemaji wa klabu hiyo Haji Manara, ameeleza kuwa mpaka sasa wamepokea maombi ya makocha zaidi ya 100 wanaotaka kuchukua nafasi ya Patrick Aussems.

'Tumefanya mazungumzo na shirikisho la kandanda nchini TFF ili abaki na klabu yetu ya Simba aendelee kuinoa kwasababu awali alitakiwa kusafiri na timu ya taifa ya Tanzania Bara 'KIlimanjaro Heroes' ambayo inakwenda kushiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup nchini Uganda na yeye ni kocha msaidizi wa timu hiyo', amesema Manara.

Seleman Matola

Simba ilimfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Mbelgiji Patrick Aussems wiki iliyopita na kumpa nafasi kocha msaidizi Dennis Kitambi kuwa kaimu kocha na sasa ipo mbioni kumtangaza Seleman Matola kuwa kocha msaidizi.