Jumatatu , 12th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Simba inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki wiki hii, ikiwa ni katika maandalizi ya michuano ya kimataifa mwishoni mwa mwezi huu.

Simba SC

Simba itacheza na klabu ya Big Bullets ya nchini Malawi Ijumaa ya wiki hii katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Timu za ligi kuu Tanzania bara (TPL) ziko mapumziko ya wiki moja hivi sasa kupisha michuano ya kimataifa, ambapo wachezaji kadhaa wa Simba wakijumuishwa katika kambi ya Taifa Stars iliyojichimbia nchini Afrika Kusini.

Simba imepangwa na klabu ya Mbabane Swallows ya Botswana katika mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika. Wapinzani hao wa Simba ndiyo walioitoa Azam Fc katika michuano ya shirikisho miaka miwili iliyopita.

Azam Fc ilishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam kabla ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 nchini Botswana katika mchezo wa marudio na hatimaye Azam Fc kuondolewa kwa uwiano wa mabao 3-1.