Alhamisi , 2nd Jul , 2020

TFF yatangaza nusu fainali ya Azam Sports Federation CUP kuchezwa Julai 11 na 12, jijini Tanga na Dar es salaam.

Hekaheka uwanjani katika mmoja ya mchezo baina ya watani wa jadi Simba na Yanga(Pichani)

Baada ya hapo jana kukamilika kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Azam Sports Federation CUP na kushuhudia timu za Sahare All Stars na Simba Sc zikiungana na Yanga sc na Namungo FC katika hatua ya nusu fainali, hii leo shirikisho la soka TFF limetangaza tarehe 11 na 12 ndio itachezwa michezo ya nusu Fainali.

Nusu fainali ya kwanza itachwa julai 11 uwanja wa mkwakwa jijini Tanga, Sahare All Stars timu ya daraja la kwanza watakuwa wenyeji wa Namungo fc ya mkoani Lindi, mchezo huo utachezwa saa Tisa alasiri.

Katika hatua ya Robo fainali Sahare All Stars iliitoa Ndanda FC ya mtwa kwa mikwaju ya penati 4-3, wakati Namungo walitinga hatua hii baada ya kuinyuka Allliance Fc ya mwanza mabao 2-0.

Julai 12 itachezwa nusu fainali ya pili uwanja wa taifa Dar es salaam ambapo mabingwa wa Tanania bara Simba SC watakuwa wenyeji Yanga sc mchezo huu utachezwa majira ya saa kumi na moja jioni.

Simba wametinga nusu fainali baada ya kuwaondoa mabaingwa watetezi Azam Fc kwa mabao ushindi wa mabao 2-0 wakati Yanga waliiondoa Kagera Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

 

Fainali ya Azam Sports Federation cup itafanyika uwanja wa Nelson Mandela Sumba Wanga mkoani katavi.