
Simba SC na Yanga SC
Klabu ya Yanga imeandika kupitia mitandao yake ya kijamii,
‘’Uongozi wa klabu ya Yanga umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17-03-2021. Kwa niaba ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga tunatoa pole kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Mhe.Samia Suluhu.’’
kwa upande wa klabu ya Simba nayo imetuma salama zake za pole ambapo taarifa ya mabingwa hao wa Tanzania imesema
‘’Uongozi wa klabu ya Simba Umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambacho kimetokea Jana Jumatano Machi 17, 2021 kwenye hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es salaam. Katika kipindi hiki ambacho watanzania bado tupo kwenye huzuni kubwa ya kumpoteza kiongozi wetu wa kitaifa, tunawaomba watu wote tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Tunatoa pole kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Mhe. Samia Suluhu, familia, ndugu, jamaa na watu wote ambao wameguswa na msiba huu mzito.’’
Klabu ya Azam FC nayo metuma salam zake za pole kwa viongozi na watanzania kwa ujumla,
‘’UongozI wa Klabu ya Azam, umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kilichotokea jana Jumatano Machi 17, 2021.
Akilihutubia Taifa usiku wa Machi 17, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, alisema Rais Magufuli alifariki katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam, majira ya saa 12:00 jioni kutokana na tatizo la moyo. Kwa niaba ya wafanyakazi wetu wote, mashabiki na wapenzi, tunatoa pole kwa Makamu wa Rais, Mh. Samia na Serikali kiujumla, Watanzania, ndugu, jamaa na marafiki, kwa kumpoteza kiongozi huyo shupavu wa Taifa.
Azam FC tunaungana na Watanzania wote kuomboleza kifo cha mpendwa wetu, kwa kutambua na kuheshimu mambo makubwa aliyolifanyia Taifa hili kwa muda wote aliohudumu ndani ya Serikali. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, ailaze roho ya marehemu, mahala pema peponi, Amen.’’