Jumanne , 4th Oct , 2022

Klabu ya Simba itaondoka nchini Oktoba 08, 2022 kueleka nchini Angalo ambako itacheza mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao Primeiro de Agosto, mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza utakaochezwa Oktoba 09,2022. Amethibitisha Afisa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally.

Kikosi cha Simba kitaondoka nchini Jumamos kwenda Angola kucheza mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Primeiro de Agosto

Kwa mujibu wa ratiba yao ya maandalizi Ahmedi amesema kikosi kinaingia kambi leo Jumanne tayari kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya de Agosto, na ameweka wazi kuwa kikosi kitaondoka nchini siku ya Jumamosi Oktoba 8 siku moja kabla ya mchezo, na baada ya mchezo kumalizika siku ya jumapili wataanza safari ya kurejea nyumbani.

Wakati kikosi hicho kikiwa kinaanza maandalizi hayo wataendelea kuwakosa wachezaji watatu Jimmyson Mwanuke, Shomari Kapombe na Peter Banda hawa wote wana majeruhi. Simba wanaelekea kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kushinda mchezo wa Ligi kuu NBC Premier League dhidi ya Dodoma Jiji kwa mabao 3-0 na sasa wanaongoza Ligi.