Jumamosi , 19th Feb , 2022

Kikosi cha Simba SC kimefika salama nchini Niger leo jioni tayari kwa mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao US Gendarmerie. Timu hizi mbili zitashuka dimbani kesho kuwania alama 3 katika muendelezo wa michezo ya hatua ya makundi.

Golikipa wa Simba Aishi Manula wakiwa uwanja wa ndege nchini Niger

Kikosi cha Simba SC kiliondoka jijini Dar es salaam jana majira ya Saa 11 jioni kikiwa na wachezaji 23 pamoja na viongozi. Mchezo huu utachezwa kesho majira ya Saa 1:00 Usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania katika uwanja wa Stade Général Seyni Kountché uliopo mji mkuu wa Niger Niamey.

Mchezo huu ni wa pili kwenye michezo ya hatua ya makundi na timu hizi zimepangwa Kundi D, Mchezo wa kwanza Simba iliifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast mabao 3-0 wakati Gendarmeri wao walifungwa ugenini na RS Berkane mabao 5-3.