Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Simba, Charles Ilanfya (Kulia pichani) akipokea Mkataba kutoka kwa Kocha msaidizi wa mabingwa hao wa Nchi , Seleman Matola (Kulia Pichani).
Nyota huyo ambaye aliwahi kuichezea Mwadui ya Shinyanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia miamba hiyo ya soka hapa nchoni Tanzania.
Kabla ya kujiunga na Simba, Ilanfya ameitumikia KMC kwa msimu mmoja, ingawa kabla ya kutua KMC aliwahi kuwaniwa na Klabu ya Yanga kufuatia mapendekezo ya aliyekua kocha wa kipindi hiko Mwinyi Zahera lakini mpango hup haukukamilika.
Katika taarifa ya Klabu ya Simba, kupitia mitandao yake ya kijamii, imearifu kuwa usajili huo ni kutokana na mapendekezo ya kocha wao mkuu Sven Vandenbroeck ambaye alisema kuwa Ilanfya atakua msaada mkubwa kwa timu yao na Taifa kwa ujumla.






