
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC
Vinara vya ligi hiyo kwenye msimamo mwa msimu wa 2016/17, Simba SC watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati mabingwa watetezi wa taji hilo Young Africans itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Africans Lyon pia ya Dar es Salaam itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati Maafande wengine kutokea mkoani humo JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ambapo Ndanda itawakaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa Simba
Ligi hiyo itaendelea Alhamisi Novemba 3, mwaka huu kwa michezo miwili ambayo itafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Mwadui kuialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex huko Shinyanga huku Mbao FC ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Wakati ligi hii ikiingia ukiongoni kwa nusu msimu, TFF inatoa wito kwa timu kujiandaa na dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuanza Novemba 15, mwaka huu kusajili wachezaji mahiri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwendelezo wa ligi hiyo nusu ya msimu uliobaki utakaoanza baadaye Desemba.
Wakati wa usajili wa dirisha dogo ndipo michuano ya hatua ya awali ya kuwania Kombe la Shirikisho 2016/2017 inatarajiwa kuanza Novemba 19, mwaka huu ambako pia imepangwa kuzindua michuano hiyo huko mkoani Mara.
Safari hii timu shiriki zimeongezwa kwa kujumuisha mabingwa wa mikoa wa mwaka jana hivyo kufikisha idadi ya timu 86 badala ya 64 za msimu ulioipita.