
(Mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo Nchini, Yusuph Singo)
Singo ameyasema hayo leo Disemba 16, 2021 baada ya kumalizika kwa fainali ya mchezo wa Netiboli ambapo Mjini Magharibi Unguja wameibuka Mabingwa kwa kuonyesha ushindani mkubwa mbele ya timu ya Mkoa wa Dar es Salaam mechi iliyomaziki katika uwanja wa ndani wa Taifa.
“Kwa jinsi nilivyoona timu ya Mjini Magharibi ilivyoleta ushindani imedhihirishi jinsi gani nchi hii ina vipaji vingi, kupitia mashindano haya ya Taifa Cup, makocha wa timu za Taifa ikiwemo mchezo wa Netiboli kuona wachezaji wazuri,”. Amesema Singo.
“Baada ya mashindano haya Serikali ina mapango wa kuendeleza mchezo huu ili kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano ya kimataifa hapo baadae,” akamaliziai hivyo Mkurugenzi huyo.
Kocha wa Mjini Magharibi Unguja, Ramadhani Zimbwe amessema siri kubwa ya kutwaa ubingwa huo ni wachezaji wake kujituma na kucheza kitimu inawasaidia kufikia malengo hayo.
Amesema matarajio yao makubwa yalikuwa ni kupambana kucheza fainali na lengo hilo limetimia kwa kutwaa ubingwa wa kombe la Taifa Cup
“Niwapongeze wachezaji wangu wamepambana na kupigania kile kilichotuleta Dar es Salaam, kwamba kupigania katika kila hatua, wapinzani wetu (Dar es Salaam) walikuwa wagumu lakini wachezaji walifuata kile tulichowaelekeza na kuwa Mabingwa,” Amesema Zibwe.