Jumamosi , 11th Dec , 2021

Mchezo wa kundi G wakumalizia hatua ya makundi uliopaswa kufanyika siku ya Alhamisi na kuhairishwa baina ya Tottenham Hotspur dhidi ya Rennes kutokana na asilimia kubwa ya wachezaji wa Spurs kukumbwa na  maambukizi ya Uviko 19 hautachezwa tena kwa mujibu wa taarifa ya UEFA .

(Kocha wa Spurs, Antonio Conte)

Siku ya jumatano klabu ya Spurs ilitangaza kuhairishwa kwa mchezo wake dhidi ya Rennes kutokana na kuwepo kwa maambukizi 13 ya Uviko 19 kwenye timu yao   huku klabu ya Rennes wakipinga vikali wakiita ulikuwa ni uamuzi binafsi kuliko wa pamoja,

"Uefa kwa kushirikiana na vilabu vyote viwili tumejitahidi  kupata suluhu ya kuupanga upya kwenye kalenda mchezo huu lakini juhudi zote tulizozifanya  hazijaweza kupata  suluhu iliyokubaliwa na vilabu vyote, matokeo yake mchezo hautoweza kurudiwa kuchezwa” UEFA  wamesema.

Tayari Rennes wamefuzu kwenda hatua ya 16 bora   huku klabu ya Vitesse wakikamata nafasi ya pili baada ya kumfunga klabu ya NS Mura huku Spurs wakishika nafasi ya tatu.

Mchezo huu ambao  ulipangwa kuchezwa Dec 31,  sasa maamuzi ya mchezo huo  yataamuliwa  na kamati ya maadili na nidhamu ya UEFA wiki ijayo. 

Wachezaji nane wa Spurs walikutwa na maambukizi ya Uviko 19   huku sheria za UEFA zikisema kama kuna wachezaji 13 wapo  vizuri  kiafya na golikipa akiwepo basi mchezo unapaswa kuchezwa .