Jumatatu , 25th Jan , 2016

Bingwa wa zamani wa michuano ya tennis ya wazi ya Australia Stan Wawrinka ametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa jumla ya set 3 kwa 2 na Mcanada Milos Raonic.

Bingwa wa zamani wa michuano ya tennis ya wazi ya Australia Stan Wawrinka ametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa jumla ya set 3 kwa 2 na Mcanada Milos Raonic.

Wawrinka ambaye ni mshindi wa michuano hiyo mwaka 2014 licha ya kupambana kujinusuru katika mchezo wa leo na kulazimisha kwenda hadi seti tano, alijikuta akipigwa set 6-4 6-3 5-7 4-6 6-3.

Kwa matokeo ya mchezo huo ambao umetumia saa 3 na dakika 44, Raonic, mwenye umri wa miaka 25 ametinga robo fainali ya michuano hiyo.

Kwa upande wa wanawake, bingwa mara mbili wa michuano hiyo Victoria Azarenka amefuzu robo fainali kwa kumchapa Barbora Strycova set 6-2 6-4, Huku Johanna Konta akimfunga Ekaterina Makarova na kuwa mcheza tennis wa kwanza wa kike kutoka Uingereza kutinga robo fainali ya michuano ya Grand Slam katika kipindi cha miaka 32 iliyopita, mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 1984.

Andy Murray pia amemfunga Bernard Tomic na 6-4 6-4 7-6 na kutinga robo fainali wakati David Ferrer akimchapa Isner kwa set 6-4, 6-4, 7-5.

Michezo ya Robo fainali kwa wanaume inaanza kesho ambapo Novak Djokovic atacheza na Nishikori wakati Roger Federer akikutana na Tomas Berdych.

Andy Murray atakutana na David Ferrer wakati Milos Raonic akikutana na mfaransa Gaels Monfils.

Kwa upande wa wanawake, Serena Williams atacheza na Maria Sharapova, Agnieszka Radwanska atacheza na Carla Suarez Navarro, Angelique Kerber akikutana Victoria Azarenka.