Ijumaa , 18th Jul , 2014

Kocha stars asema ana wachezaji sita mpaka saba wenye uwezo wa kufunga magoli ndani ya dakika moja na sasa ametoa nafasi kwa wachezaji wote kucheza kwa uwezo wao na kila mmoja amwezeshe mwenzie kufunga

Kikosi cha taifa stars ambacho kitaivaa Msumbiji jumapili wiki hii.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania taifa stars mdachi Mart Nooij amesema kikosi cha timu hiyo kiko tayari kwa mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Mambas ya msumbiji mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Nooij amesema amewapa fulsa wachezaji wa timu hiyo kuonyesha uwezo wao na kupata matokeo ambayo yatawarahisishia katika mchezo ujao utakaopigwa huko Maputo baada ya wiki mbili, amesema kila kitu katika suala la maandalizi kimekamilika na anamategemeo wachezaji watafuata maelekezo yake na kuwapa furaha watanzania siku hiyo,

Nao wachezaji tegemeo wa timu ya taifa stars wanaocheza nje ya nchi Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamesema wanajua watanzania wote wanaimani kubwa sana na wachezaji wa timu hiyo hasa wakiwategemea saan wao ambao kwa hivi sasa wanacheza nje ya nchi kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha ushindi wa taifa stars

Aidha wachezaji hao wamesema dawa pekee ya kuhakikisha timu inavuka katika hatua hiyo ni kuifunga Msumbiji idadi kubwa ya magoli na kujiweka katika mazingira mazuri katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo nchini Msumbiji.