Jumapili , 28th Jul , 2019

Leo ndiyo siku ya Watanzania kulipa kisasi kwa Wakenya katika soka hasa baada ya kumbukumbu mbaya ya kichapo walichokipata katika michuano ya AFCON.

Taifa Stars dhidi ya Harambee Stars

Safari hii ni katika kuwania kufuzu michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani, ambapo Taifa Stars itawakaribisha Harambee Stars leo jioni katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo, klabu ya soka ya Simba imeahidi kutoa kiasi cha Shillingi milioni 10 kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo wataibuka na ushindi katika mchezo huo.

Baada ya mchezo huo, Stars itasafiri hadi Nairobi kucheza mchezo wa marudiano na timu itakayoshinda hapo itakuwa na uwezekano mkubwa wa kuvaana  na Sudan.